Ijumaa 26 Septemba 2025 - 13:33
Nafasi na Daraja la Wenye subira ya Kweli juu ya Imam Mahdi (aj)

Hawza/ Kwa sababu ya hali maalumu inayowakumba watu waliopo katika zama za kusubiri, iwapo watakuwa na subira ya kweli, watapata hadhi na cheo cha thamani kubwa mno.

Shirika la Habari la Hawza - Katika mafundisho yenye thamani ya Maimamu Ma‘sumin (as), nafasi na hadhi kubwa mno imetajwa kwa ajili ya wanaomsubiria kwa dhati Imam Mahdi (aj) kiasi cha kwamba kwa hakika ni jambo la ajabu na lenye kushangaza, na linazua swali hili: inawezekanaje hali hiyo ikawa na thamani ya juu kiasi hicho? Sasa tunanukuu baadhi ya fadhila na ubora kwa wanaosubiri kwa kutumia riwaya za Maimamu Ma‘sumin (as).

1- Ni watu walio bora zaidi

Kwa sababu ya hali maalumu inayowakumba watu waliopo katika zama za kusubiri, iwapo watakuwa na subira ya thati, basi watapata hadhi ya thamani kubwa sana.

Imam Sajjad (as) kuhusu jambo hili anasema:

إِنَّ أَهْلَ زَمَانِ غَیْبَتِهِ وَالْقَائِلِینَ بِإِمَامَتِهِ وَالْمُنْتَظِرِینَ لِظُهُورِهِ عجل الله تعالی فرجه الشریف أَفْضَلُ مِنْ أَهْلِ کُلِّ زَمَان لِأَنَّ اللَّهَ تَعَالَی ذِکْرُهُ أَعْطَاهُمْ مِنَ الْعُقُولِ وَ الْأَفْهَامِ وَ الْمَعْرِفَةِ مَا صَارَتْ بِهِ الْغَیْبَةُ عَنْهُمْ بِمَنْزِلَةِ الْمُشَاهَدَةِ

Hakika watu wa zama za ghaiba yake, ambao wanaamini katika uimamu wake na wanasubiria kudhihiri kwake, ni bora kuliko watu wa zama zote; kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amewapa akili, ufahamu na maarifa kiasi kwamba ghaiba kwao imekuwa sawa na kushuhudia.
(Kamal al-Din wa Tamam al-Ni‘mah, Juz. 1, Uk. 319)

Ni wenye kuhudhuria katika hema lake wakati wa kudhihiri

Miongoni mwa matamanio makuu ya watu wema wote ulimwenguni, ni kushiriki katika zama ambazo hazitakuwa na ufisadi, dhulma na uharibifu, fadhila hii inafikia ukamilifu wake wakati ambapo mtu anakuwa katika zama za kudhihiri, katika nafasi ya karibu zaidi na kiongozi wa harakati, yaani hema lake tukufu.

Imam Sadiq (as) akiwaelezea wanaosubiri kwa dhati ambao hawatadiriki zama za kudhihiri, anasema:

مَنْ مَاتَ مِنْکُمُ عَلی هَذا الْاَمْرِ مُنتَظِراً کانَ کَمَنْ هُوَ فِی الفُسْطَاطِ الَّذِی لِلْقائم

Yeyote miongoni mwenu atakayekufa katika hali ya kusubiri jambo hili, ni sawa na yule aliye katika hema la Imam al-Qaim.
(Kafi, Juz. 5, Uk. 22)

Thawabu zao ni sawa na malipo ya mwenye kuswali na kufunga

Miongoni mwa ibada bora kabisa ni swala na swaumu, riwaya zinaonesha kwamba endapo mtu ataumaliza umri wake katika kusubiria kudhihiri Imam (as), basi malipo yake ni sawa na mwenye kuswali na kufunga.

Imam Baqir (as) kuhusu jambo hili anasema:

وَاعْلَمُوا اَنَّ المُنتَظِرَ لِهذا الاَمْرِ لَهُ مِثْلُ اَجْرِ الصَّائِمِ القائِمِ

Jueni kwamba, hakika thawabu ya mwenye kusubiri jambo hili ni sawa na thawabu ya mwenye kufunga na kufanya ibada ya usiku.
(Kafi, Juz. 2, Uk. 222)

Ni wenye heshima zaidi katika umma na marafiki wa Mtume (saww)

Kati ya wanadamu, ni nani aliye bora kuliko Mtume Mtukufu wa Uislamu (saww) ambaye ndiye bora wa mitume wa Mwenyezi Mungu na kiumbe kipendwacho zaidi mbele ya Allah? Sasa, yule ambaye katika zama za kusubiri ataishi ipasavyo, atakuwa miongoni mwa watu wenye heshima zaidi katika umma wa Mtume na atakuwa karibu naye, kama ambavyo Imaam mwenyewe (as) amesema:

اُولئِکَ رُفَقائی وَاکْرَمُ اُمَّتی عَلَی

Hao ni marafiki zangu na watu wa heshima zaidi katika umma wangu.
(Kamal al-Din wa Tamam al-Ni‘mah, Juz. 1, Uk. 286)

Mujahidina katika njia ya Mwenyezi Mungu pamoja na Mtume (saww)

Miongoni mwa wanadamu wenye heshima zaidi ni wenye kupigana jihadi katika njia ya Allah, fadhila hizi zinafikia ukamilifu wake pale inapokuwa ni jihadi pamoja na kusuhuniana na mwanadamu mkamilifu, yaani Mtume Mtukufu wa Uislamu (saww).

Imam Hussein (as) anasema:

إِنَّ الصَّابِرَ فِی غَیْبَتِهِ عَلَی الْأَذَی وَالتَّکْذِیبِ بِمَنْزِلَةِ الْمُجَاهِدِ بِالسَّیْفِ بَیْنَ یَدَیْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وآله

Hakika anayevumilia maudhi na kudhalilishwa katika zama za ghaiba, ni sawa na mujahid anayepigana kwa upanga mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saww).
(Uyun Akhbar al-Ridha (as), Juz. 1, Uk. 68)

Ni wenye malipo ya mashahidi elfu moja miongoni mwa mashahidi wa mwanzo wa Uislamu

Kuhusu ubora wa wanasubiri kwa dhati na waliothabiti juu ya wilaya ya Ahlul-Bayt (as), imesemwa kwamba watapewa thawabu zinazozidi mashahidi elfu moja wa mwanzo wa Uislamu.

Imam Sajjad (as) kuhusiana na jambo hili anasema:

مَن ثَبَتَ عَلی مُوالاتِنا فِی غَیْبَةِ قائِمِنا اَعْطاهُ اللَّهُ عَزَّوَجَلَّ اَجْرَ اَلْفَ شَهیدٍ مِنْ شُهَداءِ بَدْرٍ وَاُحُدٍ

Yeyote atakayebakia thabiti juu ya mapenzi yetu katika kipindi cha ghaiba ya Qaim wetu, Mwenyezi Mungu Mtukufu atampa thawabu ya mashahidi elfu moja miongoni mwa mashahidi wa Badr na Uhud.
(Kamal al-Din wa Tamam al-Ni‘mah, Juz. 1, Uk. 323)

Utafiti huu unaendelea...

Imenukuliwa kutoka katika kitabu kiitwacho: “Darsname-ye Mahdawiyyat” kilichoandikwa na Khodamrad Salimiyan, huku ikifanyiwa mabadiliko kiasi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha